Mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe Jokete Mwegelo ametoa majumuisho ya Harambee ya TOKOMEZA ZERO kwa kuitaka jamii kuelewa kuwa kumuelimisha mwanamke ni ukombozi kwa karne ya 21 ambayo kila mwanamke anatakiwa kuwa na elimu yenye tija na manufa kwenye mfumo bora wa maisha ya kila siku ambayo ni mpango mkakati wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM),
Akitoa wito huo kisarawe alipokua akiongea na wanahabari alipokua akitoa tadhimini ya harambee kwa michanganua mbalimbali ambapo jumla ya shilingi milioni mia tisa na kumi na tano elfu na laki moja na sabini na nne elfu zilikua zimepatikana na milioni themanini na laki sita arobaini na moja elfu zimepokelewa taslim na zipo bank,
Aidha Mwegelo alitoa ushauri kwa jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa hali na mali ili kuweza kuisaidia jamii hasa ya vijijini ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi za kuweza kuwarudisha nyuma kimaendelea wanawake na watototo wa kike,
‘’kiujumla jamii yetu inapitia mambo mengi ya kuweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo hivyo tukishikamana kwa pamoja tunamsaidia mwammke wa kitanzania, ’’alisema Mwegelo
Jumla ya ekari ishinini na Nane za mraba za shule hiyo zitatumika kwa shule hiyo na Michango yote hiyo inayokusanywa inategemea kujenga shule ya kisasa ya kihistoria ya wasichana pekee kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita Kisarawe Tarafa ya Sungwi ya Kibuta kijiji cha Mhaga.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa