Katika kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo kisarawe mkuu wa wilaya Mhe jokete Mwegelo ameitka jamii ya kisarawe kushiriki kwa vitendo katika ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ili jamii iondokane na ujinga na kupata mafanikio ya haraka akizungumza hayo katika zoezi la uhamasishaji wa jamii kushrikiki katika ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ikiwemo madarasa na matundu ya choo katika kijiji cha vihingo Kata ya Vihingo na Mzenga
‘’ifike wakati sisi jamii ndio tuwe wa kwanza kuanzisha miradi kisha ndio serikali iwekeze nguvu zake sasa ndio wakati wa sisi vihingo na mzenga kujitolea kupata miundo mbinu hii bora ya elimu hapa tarafa ya mzenga na kisarawe’’ alisema Jokete
jamii inaposhiriki ipasavyo na kwa vitendo katika ujenzi wa miundo mbinu ya elimu huwa chachu ya kupata kilicho bora kabisa maana jamii huwa na uchungu nacho kutokana kuwekeza nguvu zao na huwa walinzi wakubwa hivyoo nitoe wito kwa wana kisarawe wote kuwa tayari kujitolea kwa hiari,
‘’Nawagiza watendaji wa vijiji na kata kwa wale wote watakao kata kujitolea katika ujenzi huu wa taifa katika vijiji na kata ambao mradi ulipo fuateni sheria ndogo za vijiji zilizotungwa katika jamii zetu kwa weledi kabsa ili kufikia nlengo la mradi kwa jamii kushiriki sawa’’ alisisitiza jokete
Jumla ya bilioni moja zimetolewa kwa ajili ya shule ya msingi kola,mzenga, masaki,luhangai,vihingo na shule ya sekondari mzenga kimani,kibuta ambazo fedha hizo zinatokana na mradi wa Lipa kulingana na matokea P4R (pay for result)
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa