DC JOKETE,DK KIHAMIA ‘’WANANCHI KISARAWE KIBUTA JITOKEZENI KWA WINGI KATIKA KUANDIKISHWA DAFTARI LA UCHAGUZI’’
Mkuu wa Wilaya Kisarawe Jokete Mwegelo ametoa wito wa kila raia mwenye sifa ya kupiga kura kuandikishwa katika daftari la kupiga kura linaloanza kuandikishwa Kisarawe katika tarafa ya sungwi kata kibuta kwa muda wa siku saba kujitokeza kuandikishwa na wanachi wafuate sheria na kanuni ili wapate haki ya kuandikishwa katika daftari hilo la taifa,
Aidha ametoa wito kwa watalam wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuendana na kasi na ufanisi wa kuandikisha watu kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kuwaacha watu wenye sifa za kuandikishwa katika daftari la wapigakura,
‘’imani yangu Nec mtatenda haki na watalamu watakua na kasi ya kuandikisha raia vizuri ili kuepusha manunguniko ya raia kuachwa katika kuandikishwa, ’’ alisitiza Jokete
Nae mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi Dk Athuman Kihamia alimhakikishia mkuu wa wilaya kuwa watalamu wake watafanya kazi hiyo kwa uweledi mkubwa hasa ikizingatiwa tume yangu ina vifaa bora na vya kisasa kwa kazi hiyo ya uandikishaji daftari la wapiga kura.
‘’Nikutoe hofu mheshimiwa mkuu wa wilaya vijana wangu wapo makini na watafanya kazi hii kwa weledi mkubwa na watazingatia mda ulio pangwa muhimu wanachi wa kisarawe kibuta wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha zoezi hili ni bure sio kwa pesa ila ni la muda mfupi mno’’ alisisitiza Dk Kihamia
‘’KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM’’
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa