DC MAGOTI APOKEA HATI HATI ZA KIMILA KUTOKA TANAPA
Mkuu wa wilaya ya kisarawe mhe Petro Magoti leo tarehe 29-07-2025 amepokea hati za kimila kwa vijiji vitano vya Tarafa ya chole Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa urasimishaji wa mipaka kati ya maeneo ya hifadhi na makazi ya wananchi.Akipokea hati hizo leo kutoka kwa COI-I.J.Epimack afisa mahusiano jamii wa tanapa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, amefuraishwa na kitendo hicho za kupokea hati hizo 1562.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa hati hizo Mhe. Petro Magoti ameishukuru TANAPA kwa hatua hiyo muhimu na kueleza kuwa hati hizo zitasaidia kuondoa migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu. Alitoa wito kwa wananchi wa vijiji husika kuendelea kushirikiana na Serikali katika kulinda maeneo ya hifadhi na kutumia ardhi kwa shughuli endelevu za maendeleo ya kijamii kwa ujumla
Kwa upamde wake Afisa Mahusiano Jamii wa Tanapa Ndg Epimack alisema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi za kuhakikisha jamii zinazoishi jirani na hifadhi zinakuwa na usalama wa umiliki wa ardhi na kunufaika na shughuli za maendeleo bila vikwazo vya mipaka. Aliongeza kuwa TANAPA itaendelea kushirikiana na viongozi wa wilaya na vijiji ili kuhakikisha ustawi wa wananchi unazingatiwa.
Inakadiliwa watu 1562 watanufainika na mpango huo na Vijiji vilivyonufaika na mpango huu ni pamoja na Chole samvula, Kihare, Koresa,mafumbi na kwala, Mpango huu umelenga kutoa uhakika wa kumiliki ardhi kwa wananchi, kupunguza migogoro kati ya hifadhi na jamii, sambamba na kuimarisha usimamizi wa mazingira.
Ikumbukwe makabidhiano ayo yameshuhudiwa na baadhi ya maafisa pamoja na viongozi wa serikali ya wilaya ambapo TANAPA imeahidi kufuatilia matumizi ya eneo hilo ili kuhakikisha linaendelezwa kwa mujibu wa makubalianao huku serikali ya wilaya ikiahidi kutoa ushirikianao wa karibu kwa kuhakikisha eneo hilo linanufaisha wananchi wa kisarawe
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa