*"DC NYANGASA AHAMASISHA MAENDELEO YA JAMII KATA YA KISARAWE KIMANI*
KISARAWE PWANI
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, mheshimiwa MHE FATMA NYANGASA akiwa ameambata na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe , na baadhi ya wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi,RAWASA, TANESCO na TARURA, amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Kisarawe kwenye kitongoji Cha Kimani kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzijibu.
Alipokuwa akizungumza kwenye mkutano huo tarehe 15.03.2024, MHE FATMA amewataka wananchi kuwa huru kuelezea changamoto zao kwake pamoja na kuwapatia salamu za DKT SAMIA SULUHU HASSAN Kwa Kisarawe,
Pia, amewataka wananchi wa Kimani kujitolea Zaidi Katika shughuli za Maendeleo ya Jamii hasa shule, zahanati nk kwa kutoa maeneo Yao maana Serikali ya Kijiji hawana,
*"Kwa upande anaetaka kutoa Eneo la Maendeleo kama shule na zahanati amewataka wafuate kwa kuzingatia utaratibu wanaoelekezwa na maafisa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe na ambaye hatafuata utaratibu basi afuate*" alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
Aidha, MHE FATMA *"amewataka wazazi ambao watoto zao walifaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu, lakini mpaka sasa hawajawapeleka shule huenda kwa sababu wazazi wameshindwa kuwapatia mahitaji kama vile sare za shule,wahakikishe wanawapeleka shuleni watoto hao kwani Rais Samia anajitahidi sana kujenga shule na vyumba vya madarasa, na hakuna mtoto ambaye atafukuzwa shule kwa sababu ya kutokuwa na sare.*"
Mwisho, MHE FATMA NYANGASA *amewataka wazazi kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto wao ili kuwalinda na kuepuka matendo mabaya dhidi ya watoto kama vile ukatili wa kijinsia na unyanyasaji*.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa