DC NYANGASA AONGOZA MAMIA YA WAMAMA KATIKA MAADHIMISHO YA KIWILAYA YA SIKU YA MAMA DUNIANI
Na
Mwandishi Wetu
Kisarawe DC
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Fatma Almasi Nyangasa ameongoza mamia ya wamama katika maadhimisho ya kiwilaya ya siku ya Mama Duniani.
Mhe. Nyangasa amesisitiza Wamama kusimama katika nafasi zao ili kupunguza Ukatili wa kijinsia, “ Mama akisimama katika nafasi yake ukatili wa kinsia na mmomonyoka wa maadili utapungua”
Katika hafla hiyo watoa mada mbalimbali walishiriki kwa ajili ya kutoa mada ikiwa Pamoja Elimu ya ujasiriamali, masuala ya malezi na makuzi kwa Watoto na mahusiano katika familia, Elimu ya jinsia na ukatili wa kijinsia na Elimu ya nishati bora ya kupikia.
Aidha akina mama waliohudhuria katika haflla hiyo walipata nafasi ya kuona Makala yenye kuonesha mafanikio mbalimbali katika miaka 3 ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Nyangasa alitoa zawadi mbalimbali kwa akina Mama ikiwa ni pesa taslimu kwa wamama wanaojishughurisha na ujasiriamali pamoja na vifaa mbalimbali kwa wamama wajawazito kwa ajili ya kuwasaidia pindi wakijifungua.
Aidha wamama wameishukuru hafla hiyo adhimu ambapo akina Mama waliohudhuria wamefurahi kupata elimu ya kutosha juu ya nafasi ya Mama katika jamii Pamoja na kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyo wagusa akina Mama wote Tanzania.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa