DC NYANGASA ASISITIZA USAFI WA MAZINGIRA KWA WATUMISHI KISARAWE
Kisarawe Pwani
Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA leo ameongoza usafi wa Mazingira huku akimtakia afya Njema na Baraka MHE DKT SAMIA Katika Siku ya Kuzaliwa kwa Kupanda Miti,
Akizungumza wakati wa Hafla Malumu ya kupata mti kisarawe MHE FATMA NYANGASA Pamoja na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe na wanafunzi mbalimbali wa MINAKI, Kimani pamoja na Mabalozi wa Mazingira alisisitiza usafi na upandaji Miti,
*"Binafsi leo ni Siku ya Usafi wa Kila mwisho wa mwezi sambamba na Siku ya Kuzaliwa kwa MHE DKT SAMIA SULUHU HASSAN Kwa hiyo sote Hapa tuliopo tunamtakia kheri na afya Njema Katika kutuongoza Tanzania kwa ishara ya Kupanda Miti mbalimbali Hapa kisarawe*" alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
*"Watumishi mbalimbali wa kisarawe muongoze jitihada za Usafi wa Mazingira Katika jamii zetu ili tuendelee kuwa mfano kwa watu tunaoishi nao*" alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa