DC NYANGASA ATAKA MIRADI YA MAENDELEO KISARAWE KUISHA KWA WAKATI
Na
Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh Fatma Almasi Nyangasa tarehe 02/10/2023 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kufanya kikao cha hadhara na wananchi wa maneromango.
Ziara yake alianzia kata ya marui katika Shule ya secondary Kisangire akafanya ukaguzi wa mabweni ambayo yanendelea na ujenzi pamoja na miundombinu mbalimbali ya Eneo la shule,katika Shule ya msingi kisangile alifanya,
Aidha Katika alipokua hapo alikagua madarasa 4 na vyoo Vinavyo jengwa kwa mradi wa boost
Kadhalika Mhe DC Nyangasa alitembelea ofisi ya kata msanga kwa ajili ya kujionea ujenzi wa ofisi hiyo ilipo fikia
Lakini pia, alifanya ukaguzi wa bwalo la chakula shule ya sekondari maneromango
Mwisho, alifanya kikao na wananchi wa maneromango ilikusikiliza kero zao na aliwaomba pia wananchi sehemu ya kupongeza basi pia waipongeze serikali kwa ilicho fanya.
"Nasisitiza kwa wote ambao Wana Miradi Kisarawe kwa Mwaka 2022-23 Kumaliza kwa Wakati na kuzingatia kanuni na Sheria za ujenzi wa Miradi ya serikali katika Maeneo yenu "alisisitiza Mhe Nyangasa.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa