*"DC NYANGASA AWAKABIDHI MAAFISA UGANI VISHIKWAMBI HUKU AKIWAPA UJUMBE MZITO KUINUA KILIMO*"
KISARAWE PWANI
Mkuu wa Wilaya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA amewakabidhi Vishkwambi 36 Maafisa Kilimo wa Kata na vijiji na Vitongoji wa Wilaya Kisarawe na kuwataka watumie vifaa kazi hivyo kusidia wakulima kuleta tija na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao na Kilimo Kisarawe,
Zoezi la makakabidhiano ya vishikwambii hivyo limefanyima leo 27.11.2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe na akizungumza mara ya kukabidhi vishikwambi hivyo Afisa Kilimo Wilaya amesema kuwa matumizi mengine ni kusajili wakulima ambao bado hawajaingizwa kwenye mfumo na kuboresha taarifa za wale waliosajiliwa ili wahudumiwe kwa idadi na kujua mahitaji yao ya pembejeo.
"Ili kilimo kiwe na tija lazima wataalamu wawe na vifaa vya kisasa na hata iwe rahisi kutoa taarifa juu ya maendeleo ya kilimo au kama kuna changamoto," MHE NYANGASA
Amesema kuwa kupitia vifaa hivyo wtaweza kutoa taarifa sahihi za pembejeo kwa wakulima kuanzia afya ya udongo, mbegu bora, mabadiliko ya hali ya hewa na matumizi sahihi ya mbolea.
"Tunaipongeza serikali kwa kutoa Vishikwambi 36, vifaa vya kupimia udongo, hii inaonyesha jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan za kutaka kubadili kilimo ili kiwe na tija kwa wakulima na nchi,"alisisitiza MHE NYANGASA
"Zao la ufuta ubora na uzaliahaji umeongezeka na tnaongeza nguvu kwenye mazao yakiwemo Korosho ,mihogo, chikichi, mpunga na mbaazi pamoja na ndizi ambapo Kuna wakulima wameshajitokeza," alisisitiza MH NYANGASA
Ameongeza kuwa kikubwa ni maofisa hao kuongeza mnyororo wa thamani kupitia mazao ya kibiashara ambayo yanaongeza pato kwa wakulima.
Twamala amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia wakati wa kutoa taarifa mbalimbali kwa Wizara na kutoa elimu kwa wakulima juu ya masuala mbalimbali ya kilimo.
Naye afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe amesema kuwa vifaa hivyo vitawawezesha kutekeleza majukumu yao na kuongeza uzalishaji na kuleta tija kwa wakulima kwenye maeneo yao Kwa kata zote Kumi na Saba kwa maafisa 36.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa