DC NYANGASA AWATAHADHARISHA WANAOISHI MABONDENI KUONDOKA KUEPUSHA MAAFA
KISARAWE PWANI
Mkuu wa Wilaya Kisarawe MHE FATMA NYANGASA amesisitiza wale wote wanaoishi katika mabonde na milima kuondoka Mara Moja katika kipindi hiki Cha mvua zinazoendelea ili kutokupata maafa yatakayosababishwa na Madhara ya mvua 01.11.2023,
Akizungumza Wakati wa ukaguzi wa kuyabaini Maeneo ambayo hatarishi Kwa Sasa akiwa ameambatana na Kamati ya maafa ya Wilaya alisisitiza kuwa
*"Mvua hizi zinazoendelea kunyesha Maeneo mbalimbali hapa kwetu Kisarawe nitoe wito kuwa wale wote wanaoishi Maeneo hatarishi kuondoka Mara Moja bila ya shuruti ili kunusuru maisha Yako lakini pia nitoe wito watu wasiende mabondeni*" alisisitiza MHE NYANGASA
Mwisho alisisitiza zaidi kuwa watu watumie mvua hizi kwa kukaa Maeneo salama na sio hatarishi Kama mabondeni, milimani, na makorongo Nk.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa