DED KISARAWE AIPONGEZA NMB KWA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA
Na
Mwandishi Wetu
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Bi. Beatrice Rest Dominic 11-08-2023 amepokea msaada wa vifaa kutoka kwa Mdau wa Maendeleo Wilaya kisarawe bank ya NMB Tawi la Kisarawe kwa lengo kuboresha ufanisi Kazini,
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa Hivyo alishukuru Bank hiyo kwa kuona kuna haja ya kuisaidia Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe katika vifaa Hivyo ili Kuongeza ufanisi Kazini
"Binafsi nafarijika sana kwa Bank ya NMB Tawi la Kisarawe kupatia vifaa hivi ili kuboresha ufanisi Kazini alisisitiza ndugu Dominic"
"Kwa vifaa hivi mliotupatia tunawaahidi ufanisi Mkubwa na ulio tukuka hasa kipindi hiki ambacho tunapambana na kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato hapa kisarawe"
Hata Hivyo kwa upande Mwakilishi wa Meneja wa NMB Tawi la Kisarawe Bi Frida Mosha alisema kuwa ili kuboresha mahusiano Bora Baina yao na wateja Wao kama kisarawe ilibidi watoe msaada huo
"Kwa niaba ya Meneja na Uongozi mzima wa Bank ya NMB Tawi la Kisarawe tumeona tukiwapatia vifaa hivi kwenu tutaongeza zaidi mahusiano mema pamoja na kuboresha ufanisi Kazini alimalizia Bi. Mosha"
Jumla ya Kompyuta Mbili zilizokamilika walizitoa kwa Halmashauri Wilaya zikiwa tayari kwa ufanisi wa Kazi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa