DED KISARAWE ATIA SAINI MKATABA WA UTENDAJI KAZI MKOA PWANI KIBAHA.
KIBAHA PWANI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg.BEATRICE DOMINIC amehudhuria zoezi la utiaji saini wa Mkataba wa Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma kati ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zilizopo Mkoa wa Pwani na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bw.Rashid Mchatta,
Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Tarehe 16/01/2024 limeshuhudiwa na Mkurugenzi wa Uendelezaji Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Rais Utumishi Dr.Editha Rwiza,Wakuu wa idara na vitengo kutoka sektetarieti ya Mkoa pamoja na Halmashauri za Mkoa wa Pwani.
Matukio mbalimbali ya wajumbe wa Mkutano huo uliofanyika Katika ukumbi wa Mkuu wa MKOA PWANI KIBAHA.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa