*DKT JAFO AKABIDHI PIKIPIKI KWA WALIMU WANAWAKE KISARAWE*
PWANI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira MHE DKT SELEMANI SAIDI JAFO Leo amewakabidhi pikipiki Moja walimu wanawake Kisarawe kwa lengo la Kuongeza Kipato na kutunisha mfuko wao wa Shughuli za Mapato Katika Chama Chao Kisarawe,
Akizungumza Wakati wa Hafla hiyo Mhe DKT JAFO aliesema kuwa amefurahishwa na utulivu wao walimu Kisarawe ndio maana akavutiwa kuwasaidia ili kuinua mfuko wao,
*"Nikiri wazi walimu wangu nawapenda mno ila utulivu wenu katika Chama umenivutia mpaka nikamua kuwasaidia ili kuinua mfuko wenu wa Chama katika shida ndogo ndogo Kama Chama alisisitiza MHE JAFO,
Nae akizungumza Wakati wa Hafla hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha walimu Wilaya Kisarawe Mwalimu Francis Mkamba alimpongeza Mhe DKT JAFO kwa Moyo wa kukijali Chama Cha walimu Kisarawe,
*"Binafsi naomba ujue kuwa Hawa walimu Hawana Cha kukulipa ila zaidi kukuombe Dua ya kher na amani na upendo kwetu kwako maana unakijali mno Chama chetu alisisitiza Mwalimu Mkamba
Jumla ya pikipiki Moja aina ya boxer imemkabidhi kwa Chama Cha walimu Kisarawe kutoka kwa Mbunge ikiwa ni pikipiki ya Tatu kutoka kwa Ofisi ya Mbunge kwenda Chama Cha walimu kwa kazi ZAO binafsi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa