" DR JAFO ATAKA WALEMAVU WAWEZESHWE LUGHA ZA ALAMA KATIKA JAMII"
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Daktari Selemani Said Jafo ameitaka Jamii ya watanzania kuwapatia walemavu watalaamu wa lugha za alama ili nao wao walemavu kuendana na Jamii Katika kukabiliana na Mazingira Katika ujenzi wa Taifa,
Akizungumza wakati wa kupokea na kutoa vifaa vya watoto wenye ulemavu Mkoa wa Pwani Wilaya Kisarawe leo kutoka Shirika la Plan International Tanzania alisema
Natamani kutoka moyoni nionavyo me na Jamii ione hivyo kuwajali na kuwapatia walemavu watalaamu wa lugha za alama ili waweze kuyakabili maisha kuondokana na changamoto ya lugha ya alama Katika Jamii alisema Dr JAFO"
"Lugha za alama Ni kiungo Muhimu Sana kwa Mazingira ya Sasa hivyo walemavu wanapaswa kutatuliwa Hili tatizo la lugha za alama ili wapate mafanikio mazuri ya maisha kuondokana na Hili Muhimu kuwapatia vitabu, walimu,na vitendea kazi kuvipata kwa wakati aliongeza Dr JAFO"
"Nawapongeza Sana Shirika la Plan International Tanzania kwa msaada wenu huu kwa walemavu hapa Kisarawe nawaomba endeleeni kuwapatia na kuwajali watoto Hasa Hawa walemavu na Mwenyezi Mungu atawalipa alimazia Dr JAFO"
Shirika la Plan International Tanzania Kisarawe leo limekabithi vifaa hivyo kwa Mbunge wa Kisarawe ambaye pia Ni Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais vifaa venye Dhamani ya shilingi Milioni Sitini na Sita kwa ajili ya Watu watoto walemavu ikiwemo Viti vya baiskeli, Vitabu Nk.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa