Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo ametoa wito kwa Maafisa Watumishi wa Taasisi za Serikali na Mashirika yaliopo katika Mkoa wa Pwani kuwajali na kuwaonea huruma wafanyakazi wanaowasimamia Pindi wanapopokea Matatizo na Shida zao katika Maeneo yao ya Kazi ,
Akitoa wito huo katika Madhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo kimkoa zimefanyika katika Wilaya ya Kisarawe viwanja vya Shule ya Sekondari na Msingi Chanzige aliwataka kusimamia Misingi hiyo ya kiitumishi kwani hupelekea kuleta Uwiano Mzuri na Maendeleo Baina ya Pande hizo Mbili za Wafanyakazi,
Aidha Ndikilo aliwataka Maafisa hao Watumishi Kuhakikisha kuwa Wanawapatia wafanyakazi hao Elimu elekezi ya maeneo ya kazi ili kila Mfanyakazi elewe zaidi maslahi yake kwa undani Zaidi,
Mwisho alitoa kwa wafanyakazi wote wa mkoa wa pwani kuendelea kujenga nchi kwa ari ya kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ili kuendelea kuwahudumia kwa ufanisi wananchi wanaowazunguruka
’’KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO’’
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa