FURSA ZIPO TUJITOKEZE KUZITUMIA - DC NYANGASA
Na
Mwandishi Wetu.
07/03/2023
Maadhimisho ya siku ya wanawake kiwilaya yalifanyika katika viwanja vya chanzinge yenye kauli mbiu "Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia."
Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Fatma Almas Nyangasa, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya amesisitiza utumiaji wa Fursa" Fursa zipo tujitokeze tuzitumie" DC Nyangasa alisema.
Aidha Mhe. Nyangasa alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanawake wanaojituma na kufanya kazi kwa bidii na kusema kila kitu kina mwanzo, " Hata mti wa Mbuyu ulianza kama mchicha" DC Nyangasa alisema.
Maadhimisho ya siku ya wanawake yaliambatana na michezo na burudani mbalimbali.
Matukio kwa njia za Picha.
|
|
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa