MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA KISARAWE Ndg MUSSA GAMA amewataka wazazi wa kijiji cha mengwa kata ya BOGA kuwekeza katika elimu ya msingi kwa kuwasomesha watoto ili waweze kupata maarifa bora ya malezi na elimu hapo baadae akizungumza na wazazi hao wakati wa Ghafla maalum ya kuwapatia vifaa kazi na vitendea kazi kwa wanafunzi hao kijijini hapo alisema ‘’ imefika wakati sisi wazazi tuwekeze Zaidi katika mambo ya msingi kwa vijana wetu hasa watoto wa kike katika elimu bora na malezi ili taifa lije kua bora hapo baadae kwa maslah ya jamii yetu’’alisema GAMA Suala la elimu kwa vijana na watoto wa kike limekua na changamoto nyingi wilayani kisarawe hasa vijijini .
Suala la elimu limekua na changamoto kubwa zinazowakumba watoto wa kike katika kijiji cha mengwa na wilaya kwa ujumla.Miongoni mwa changamoto hizo ni kutembea umbali mrefu waendapo shuleni,mimba zautotoni,tamaduni na mila potofu ambazo huwarudisha nyuma kimaendeleo wawapo shuleni mfano kuchezwa ngoma. Changamoto nyingine ni jamii haitilii mkazo suala la elimu kiujumla kwa watoto wa kike.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa