Wazee wa Kisarawe Wapatiwa vitambulisho vya matibabu.Agizo la utengenezaji vitambulisho vya matibabu linaendelea kukamili katika Wilaya ya kisarawe. Awamu ya kwanza ya ugawaji wa vitambulisho umetolewa katika kata ya kisarawe. Vitambulisho hivi vimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Kisarawe Ndugu Musa Gama ambapo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 watakuwa wanatibiwa bure. Mhe. Abel Mudo Diwani wa kata ya kisarawe aliwasisitiza wazee kuvitumia vizuri vitambulisho hivyo wakati wa kuwagawia.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa