HONGERA SANA KISARAWE KWA KUHAKIKISHA HEWA SAFI YA UKAA NA SALAMA DAR ES SALAAM
MWANDISHI WETU
Morogoro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo amepongeza jitihada zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya kisarawe katika kuhakikisha inatunza Mazingira na kuhakikisha inafuga ng'ombe vizuri kanda Mashariki,
Mhe. Jafo, ametoa pongezi hizo leo Agosti 7,2023 alipotembelea Banda la Kisarawe kwenye maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere mkoa Morogoro Kanda Mashariki,
Aidha, ameitaka kisarawe kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzuia shughuli za kibinadamu zinazofanyika pembezoni mwa vyanzo vya maji ili kuepusha kujaa kwa uchafuzi katika msitu wa Kazimzumbwi ambalo ni chanzo mama cha hewa safi kwa wakazi wa Dare es Salaam na Pwani.
Sambamba na hilo amesisitiza juu ya utoaji wa elimu kuhusu athari ya vitendo vya uchomaji moto wa misitu iliyopo katika Milima ya Uluguru ili kuhifadhi mazingira na vyanzo maji Mkoa Morogoro,
Kisarawe inashiriki maonesho ya nanenane huku ikisogeza karibu huduma mbalimbali zinazotolewa na halmashauri hiyo pamoja na utoaji wa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya maji na utumzaji wa Mazingira,kulima Chikichi,kwa wananchi wanaojitokeza katika maonesho hayo pamoja na Kutoa elimu kuhusu ufugaji, Kilimo NK,
Aidha kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam malima alifurahishwa na Mdau wa Maendeleo wa Kilimo Cha Chikichi kutoka kampuni ya Winnamwanga cultural heritage na kumtaka abaki Morogoro baada ya Nanenane ili Kutoa elimu ya Kilimo hicho kwa Wakulima wa Morogoro,
Nae kwa upande wake pia Msimamizi wa Winnamwanga cultural heritage alikubali Ombi la mkuu wa Mkoa kubaki Morogoro ili Kutoa elimu ya kulima zaidi Chikichi za kisasa Mkoa Morogoro.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa