Katika kufikia malengo ya Dunia ya asilimia hamsini kwa hamsini ya milenia kabla ya mwaka 2020 katika ushiriki wa wanawake kwenye maamuzi ya mambo yanayowahusu ya kijamii,kiuchumi, na kimaendeleo wito umetolewa kwa wanawake KISARAWE kushiriki mikutano, kongamano, warsha na vikao vya maamuzi bila ya woga.
Akizungumza katika warsha ya kupaza sauti kwa ajili ya wanawake na watoto kwenye masuala ya haki za jamii na kiuchumi na kufanya watambue ndoto zao na malengo yao kisarawe afisa maendeleo ya jamii idaya ya mipango Ndugu Jalia B.Chanyika amesema;
‘’Ni muhimu kwa wanawake na watoto wenye mwamko wa maendeleo kupaza sauti katika mambo yanayowahusu wao kwa maslah yao wao wenyewe wasisubiri kupangiwa kwani anayekupangia hatokupangia yote yenye msingi na dira ya kukukwamua katika wimbi la usawa wa kijinsia ’alisisitiza chanyika ’
Kuelelekea kilele cha Siku ya wanawake duniani warsha na mikutano mbalimbali zimeandaliwa na kuratibiwa na idara ya maendeleo ya jamii kisarawe kwa lengo la kuwafikishia ujumbe wa kujiendeleza kimaendeleo hasa kwa kushirikisha mashirika na taasisi mbalimbali lengo ikiwa ni kumkomboa mwanamke na motto. Miongoni mwa taasisi zinazoshiriki wiki ya mwanamke duniani ni Briht jamii, Save the elder zote za Dare es salaam
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu’’ alimalizia chanyika
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa