Wilaya ya kisarawe imefanikiwa kuendesha jukwaa la uwekezaji kwa kishindo. Mgeni rasmi Mhe. Selemani Jaffo ambaye ni Mbunge wa kisarawe na Naibu Waziri OR-TAMISEMI amewakaribisha wawekezaji mbali mbali ambao walikuwa wamealikwa kwenye jukwaa hili ili kuweza kuwekeza katika Wilaya ya Kisarawe. Mhe. Naibu Waziri amesema zipo fursa nyingi sana katika Wilaya ya Kisarawe ambazo mtu anaweza kuwekeza. Amesema Wilaya ya kisarawe unaweza kuwekeza katika viwanda,kilimo,mifugo,Biashara,utalii na makazi.Pia amesisitiza kuwa ndani ya Wilaya ya kisarawe kuna maeneo ya kutosha kwa uwekezaji wa aina yeyote ile ambao Utakuwa na tija kwa mafanikio ya wananchi na Taifa kwa Ujumla. Pia amemshukuru Mhe. Raisi Magufuru kwa kuwaelekeza DAWASCO kuleta maji safi toka mto Ruvu.Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kufikia desemba bara bara nyingi za mitaa ndani ya kisarawe zitakuwa zimewekewa lami hivyo wajipange kuja kuwekeza bila wasi wasi.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Happyness W Seneda amewaomba wawekezaji waje kwa wingi kuwekeza ndani ya Wilaya ya Kisarawe. Ameseme Wilaya ya kisarawe itatoa ushirikiano mzuri kwa kila mwekezaji atakayeonyesha nia ya kuja kuwekeza.
Kupata maelezo zaidi bonyeza hapa.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa