KISARAWE - PWANI
Kikao cha Kamati ya Ushauri Wilaya (DCC) kimefanyika leo tarehe 14/12/2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, uliopo Mtaa wa Bomani, Kata ya Kisarawe, Mkoani Pwani.Katika kikao hicho Mhe. Jokate Mwegelo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alisisitiza kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni ili wapate haki yao ya msingi ambayo ni elimu, pia watendaji na wataalam wahakikishe wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, pamoja na Hotuba aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli wakati wa Ufunguzi wa Bunge.Sambamba na hilo, Mhe. Jokate alisema watendaji wawe na nidhamu katika utendaji wao wa kazi na utoaji huduma kwa wananchi, na kuepuka wasiwe chanzo cha migogoro ya ardhi, na watoe elimu ya kilimo bora kwa wananchi, pamoja na kutafuta masoko ya mazao ya misitu kwa ajili ya maendeleo ya jamii ya watu wa Kisarawe na Taifa kwa ujumla.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa