KIKAO KAZI CHA MHE. JOKATE U. MWEGELO KIJIJI CHA MARUI MNGWATA..
Posted on: February 23rd, 2021
KIKAO KAZI CHA MHE. JOKATE U. MWEGELO KIJIJI CHA MARUI MNGWATA
Tarehe 23/02/2021 Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate U. Mwegelo amefanya ziara ya kikao kazi katika kijiji cha Marui Mngwata ambacho ni maarufu kwa ajili ya zao la ndimu. Mh. Mkuu wa Wilaya amefanya kikao kwa ajili ya kutangaza kuanza rasmi kwa msimu wa kilimo katika maeneo yote ya wilaya ya Kisarawe.
Wakulima waomba elimu juu ya kilimo ili waweze zalisha mazao ya kutosha, wakulima wamekiri kuwa endapo watapatiwa elimu ya kutosha wataweza zalisha zaidi.
2.Uhitaji wa soko katika kijiji cha Marui Mngwata
Wanachi wamemuomba Mhe.Jokate soko ili kuepukana na walanguzi.
3.Uboreshaji wa Barabara
Wananchi wameomba barabara iboreshwe ili iwe rahisi kwa ajili ya kusafirisha mazao kutoka shambani.
4. Uvamizi wa mashamba.
Wakulima wamelalamika mbele ya Mhe. Mkuu wa wilaya kuhusiana na uvamizi kutokea Wilaya ya mkuranga, hivyo wameomba mipaka iwepo kuonesha mwisho wa kisarawe na Mwanzo wa mkuranga ili kuepusha uvamizi wa mashamba.
Viongozi wa kijiji cha Marui Mngwata walianisha baadhi ya mafanikio yakiwemo;
1. Ugawaji wa ekari tatu kwa kila mwanachi ili kuondoa mashamba pori.
2. Mshikamano kati ya walimu na wanafunzi katika kilimo, wanafunzi wa kijiji cha Marui Mngwata wanashilikiana na walimu na hii imesaidia kuongeza mazao ya chakula kwa wanafunzi.
Mh.Jokate aliambatana na watalaam wa Kilimo ambao walitoa ufafanuzi na kujibu baadhi ya maswali kutoka kwa wakulima, pia watalaam wa kilimo walitoa taarifa ya mikopo kwa wakulima wadogo wadogo kutoka NMB.
Mhe. Mkuu wa wilaya alisikiliza changamoto za wananchi na kuwaambia atazitatua kwa haraka ili kufanya Marui Mngwata kuwe kitovu cha uzalishaji mazao, aidhaa aliahidi kufanya tena mawasiliano na TARURA kuhusiana na Barabara.
Pia alihimiza viongozi kutembelea kijijini Marui Mngwata kwa ajili ya kutoa elimu mara kwa mara na kukataa sababu ya usafiri kuwa kikwazo cha wataalamu kufika viijini.
Pia alihimiza wakulima kufanya kazi kwa bidii.
Matumizi mzuri ya fedha na ukusanyaji mzuri wa mapato kwa kijiji kwani kuna baadhi ya watu wanakweka kulipa ushuru.
Imetolewa na Kitengo Cha TEHAMA na UHUSIANO-Kisarawe