KIKAO KAZI KATI YA MKURUGENZI MTENDAJI ,MAAFISA ELIMU KATA,WATENDAJI KATA,MAAFISA TARAFA,WALIMU WAKUU, WAKUU WA SHULE KUJADILI CHANGAMOTO NA KUPANGA MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU KATIKA WILAYA KISARAWE.
Posted on: December 17th, 2020
KIKAO KAZI KATI YA MKURUGENZI MTENDAJI ,MAAFISA ELIMU KATA,WATENDAJI KATA,MAAFISA TARAFA,WALIMU WAKUU, WAKUU WA SHULE KUJADILI CHANGAMOTO NA KUPANGA MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU KATIKA WILAYA KISARAWE.
Leo tarehe 17/12/2020 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Mussa Gama alikuwa na kikao kazi kati ya Maafisa Elimu kata,Maafisa Tarafa,Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu. Mgeni rasmi ndugu Mussa Gama alifungua kikao kwa kuwakaribisha washiriki katika kikao kazi na kuwapongeza washiriki wa kikao na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo chanya. Ndugu Gama alisema halmashauri imetumia rasilimali nyingi kuliko matokeo tuliyoyapata.
Aidha ndugu Gama alisisitiza kila mmoja awe na Ilani ya chama Tawala ili kutenda kazi kwa kufuata ilani ya Chama na kuhakikisha Ufaulu ndani ya Wilaya ya kisarawe unaongezeka .
Sambamba na hilo Ndugu Gama alinukuu usemi usemao “Fanyeni mti kuwa mzuri au Mbaya na matunda yake yatatambulika” Ni vyema tukafanyakazi vizuri ili matunda mazuri yajitangaze . Tukiwa na bidii katika kuelimisha na kufundisha wanafunzi vizuri matunda yake tutatokomeza Ziro katika shule zetu zote.
Gama alisema “ Lengo la kikao kazi ni kujadili Changamoto na kutengeneza mpango Mkakati mzuri wa kutatua Changamoto zote ili kuinua Elimu katika Halmashauri yetu ya Kisarawe”
Pia Afisa Elimu Msingi Ndugu Bane alisisitiza wakuu wa shule na walimu wakuu kusimamia nidhamu mashule kulingana na Mwongozo wa Elimu unavyowataka kufanya.Alisema Kama kutakuwa na nidhamu kuanzia kwa walimu basi hata watoto watakuwa na nidhamu na Ufaulu utaongezeka.
Katika kikao Hicho Afisa Elimu Sekondari Ndugu Patrick Gwivaha alisisitiza kufanya kazi kwa weledi ,kuwa wabunifu na kuwakumbusha watendaji wa kata ,Maafisa Elimu kata,Wakuu wa shule na walimu Wakuu kuhusu Majukumu yao na kuyasimamia.
Mgeni rasmi alimpa nafasi Mganga Mkuu wa Wilaya Ndugu Sobo ambaye aliwaomba washiriki kutoa Elimu ya Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa wanafunzi ili wajiunge kwa wingi Maana itawasaidia katika Matibabu pindi wawapo mashuleni.Aidha alisema wanafunzi wote wachunguzwe afya (Medical Examination) katika vituo vyetu vya kutolea Huduma ndani ya Kisarawe haswa kwa wale wanaoenda kuanza masomo. Pia Ndugu Sobo aliomba watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa kusimamia vituo vya kutolea Huduma vilivyopo kwenye maeneo ili kubaini kwa haraka Changamoto zilizopo na kuhakikisha wananchi wanapata Huduma stahiki.
Mwisho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe ndugu Gama aliwataka washiriki kupanga mipango ambayo itakuwa na tija Katika Swala la Elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Kuwaahidi kwamba mipango na Mikakati yote itatekelezwa na kupewa kipaumbelee.