Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka wajasiriamali wakubwa na wadogo waliopo nchini kuwekeza katika sekta zenye kuchochea maendeleo haraka katika jamii ili kuendana na kasi ya uchumi wa kati.
Aliyasema haya wakati akifungua kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi wakishiriana na Halmashauri ya Wilaya Kisarawe alipokuwa akichangia mada ya kilimo ,Biashara ,Mikopo ,kodi na uwezeshaji.
Aidha, Mhe Jafo amemtaka mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu. Mussa Gama kuandaa Miundobinu iliyo bora na salama kwa vikundi vya wajasiriamali mbalimbali vilivyopo Kisarawe kupata mikopo na misaada ili kuboresha na kuleta tija kwa jamii.
Nae Mkurugenzi wa Wilaya Kisarawe amemwakikishia Waziri Jafo kuwa wajasiria mali waliopo Kisarawe watapata mikopo kwa wakati kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuratibu mfumo mzuri na wenye tija kwa kwao.
Sambamba na hivyo leo Ndg. Gama aliwasilisha kwa Mhe. Jafo mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi milioni miamoja na saba(107,000,000/=) ikiwa ni ukamilishaji wa asilimiakumi(10%) ya mapato ya ndani ili akabidhi kwa vikundi vya Vijana,Wanawake na Watu wenye Kisarawe.
KISARAWE TUNATEKELELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa