NA
Mwandishi Wetu
Katika kutekeleza sheria na ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa vitendo Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya kisarawe leo 10.08.2023 limefanya Mkutano na kuazimia kuwatumikia Wananchi kwa vitendo,
Akiziungumza wakati wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri Zuberi Kizwezwe amewashukuru Madiwani wake kwa Kuendelea Kuonesha nia ya kuwatumikia wananchi kwa vitendo
"Binafsi nafarijika sana kuona Madiwani wenzangu wa kisarawe jinsi mnavyojitoa katika kuwatumikia wananchi kama ambavyo ilani na Sera ya Chama chetu Cha Mapinduzi kinavyosisitiza katika hili alimalizia Mhe. Kizwezwe"
"Hata Hivyo mbali na Agenda mbalimbali zilizojadiliwa lakini tumeweza kufanikisha Kumaliza mwaka salama Hivyo kama ulivyo utaratibu inatubidi tufanye uchaguzi wa Kisheria katika kuchagua Wajumbe wapya wa Kamati za Maendeleo ili kuboresha ufanisi wa Kazi zetu kama Madiwani alimalizia Mhe Kizwezwe"
Nae Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya kisarawe Bi Beatrice Dominic Kwai aliwashukuru Wajumbe wa Mkutano kwa Kumaliza salama mwaka wa Fedha 2023 hasa Kusimamia na kupata hati safi pamoja na kuboresha Hali ya Usimamizi wa mapato ya Halmashauri,
"Tupo hapa leo ndugu Wajumbe wa Mkutano Huu niwape Tarifa fupi kuwa Halmashauri mwaka 2022 imepata hati safi kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi wa hesabu wa Serikali (CAG) Kwa hili tujipongeze alimalizia Ndugu Kwai"
Mbali na hayo mengine yaliojiri ni pamoja na kujadiliwa Kwa changamoto za wananchi ikiwemo changamoto za Ardhi,maji,umeme, Kilimo ufugaji nk .
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa