Maonyesho ya NANENANE ya Mifugo yamemalizika leo kitaifa mkoani DODOMA kwa kutolewa wito kwa watanzania kufuga Ngombe wa kisasa wa nyama ili kujiongezea kipato cha familia Pamoja na kuongeza pato la taifa kutokana na kulipa KodI Kwa Serikali,
Akitoa wito huo katika maonyesho hayo Waziri mkuu wa Tanzania Mhe Kassimu Majaliwa aliwataka watanzania kujiewekeza zaidi katika ufugaji huo wa ngombe wa kisasa kwani unatija kwa mazingira haya ya sasa na unamkomboa mtanzania dhidi ya umasikini ,
“Ndugu zangu watanzia ufugaji wa kisasa unatija sana na mzuri kwa kuwa haukupelekei kuwa na mambo mengi maana unafuga kisasa na bora kabsa kuliko ule ufugaji wa kizamani ambao umepitwa na wakati ”, alisema Majaliwa
Aidha kwa upande mwengine wilaya ya kisarawe Imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la ugugaji ngombe wa kisasa wa nyama kikanda na kitaifa kwa mwaka huu 2019 na Kutunukiwa hati ya ushindi wa kwanza Kitaifa kundi la Parade Ngombe wa nyama wafugaji wakubwa na taasisi kwenye sherehe hizo zilizofanyika Dodoma.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa