Halmashauri ya wilaya ya kisarawe imenunua kifaa cha kisasa cha kupima ARDHI kinachojulikana kama SOUTH GPS.S86 [1BASE AND ROVER] kwa dhamani ya milioni aroubaini na sita laki saba kwa kwa lengo la kupima na kupanga matumizi bora ya ardhi kwa maeneo yote ambayo hayajapimwa na kupangwa kisasa na bora kwa urasimishaji na miundo mbinu ya maendeleo KISARAWE
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya kifaa hicho katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mtaalam wa kupima na kupanga MATUMIZ YA ARHI kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wilaya hiyo Afisa ARDHI na MALIASILI Ndg Mabula K.Isambula
Mabula alisema kwa sasa changamoto zote za ardhi kwa Kisarawe hasa kwa maeneo ambayo hayajafikiwa kwa kupimwa na kupangwa matumizi bora yanaenda kutatuliwa maana kifaa hichi ni mkombozi na hasa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa na wa kisasa wa kufanya kazi kwa hali ya juu kabsa
Mabula ‘’ndugu wajumbe hiki ni kifaa cha kisasa na bora kabisa kununuliwa kwa matumizi ya ardhi hapa KISARAWE Imani yangu tunaenda kumaliza na kutafua changamoto zote za ardhi kwa kufika maeneo ambayo hajapimwa na kupangwa mpaka sasa’’ alisema mabula
Kisarawe ina maeneo mengi ya kupimwa kwa ajili ya kilimo, maakazi ya kisasa, viwanda na uwekezaji, pamoja na maeneo muhimu ya matumizi ya binbandamu na wanyama ambayo hajapimwa ila kwa sasa kila Tarafa,kata na kijiji tunaenda kupima kwa kutumia wataaalam wa Halmashauri na vifaa vyetu wenyewe na sio vya kukodisha alifafafnua Mabula
‘’kupitia kifaa hiki cha kisasa sasa tunaendalea kupanga matumizi bora ya ardhi kisasarwe kwa kila eneo cha muhimu jamii kufuata taratibu zote za kupima ardhi ili kuondosha matatizo katika jamii’’
hapo mwanzo halmashauri ilikua inatumia fedha nyingi kwa kukodisha vifaa hivi kwa sekta na wapimaji binafsi ila kwa sasa suala hili litasimamiwa na idara ya ardhi kwa vifaa vyetu wenyewe
Awali kata za kisarawe, msimbu, kazimzumwi na kiluvya ziliweza kupanga na kupima kwa baadhi ya vitongoji vyake kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi kwa kutumia watalaam wa sekta binfsi kulikopelekea kwa kupatikana kwa badhii ya maeneo ya viwanda na uwekezaji kwa baadhi ya kata hizo ambazo kwa sasa zipo katika mamlaka ya mji mdogo kisarawe
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa