Katika kufikia uchumi wa viwanda na hatua za halmashauri kubuni njia za kuongeza mapato yake ya ndani kwa mujibu wa agizo la Ofisi ya Waziri Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imeanzisha kiwanda cha kufyatua tofali za umeme zenye ubora wa kiwango cha serikali kinachotakiwa ili kukuza pato la ndani pamoja na kuhakikisha miradi ya serikali inajengwa katika ubora wa kiwango unaohitajika ,
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Kisarawe Katibu wa kikosi kazi cha mapato (KKM) Ndg James Chitumbi, alisema kwa sasa wameamua kufikia hatua hiyo ya ujenzi wa kiwanda cha matofali cha kisasa Kisarawe ili kwendana na kasi ya uchumi wa viwanda na kuongeza tija ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwani huko katika ujenzi wa kiwanda hicho cha tofali kuna fursa kubwa ya Halmashauri kupata mapato,
‘Sisi kikosi kazi jukumu letu kubwa ni kuhakikisha Halmashauri inakusanya mapato kwa kiasi kikubwa hivyo ni lazima kumshauri Mkurugezni katika kubuni na kuanzisha chanzo cha mapato hasa hiki kiwanda cha kiwanda cha kufyatua tofali ambacho kinazalisha tofali za kisasa zenye kukidhi vigezo vyote vya ujenzi wa majengo ya serikali’ alisema Chitumbi
Jumla ya miradi tisa katika sekta ya elimu na afya Kisarawe inategemea kuzitumia tofali hizo kwa mujibu wa Chitumbi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa