*KISARAWE YAJIPANGA KUPOKEA WANAFUNZI WAPYA DC NYANGASA ATOA WITO WAZAZI NA WALIMU KUSHIRIKIANA*
Kisarawe-Pwani
Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA A. NYANGASA ametoa wito kwa wazazi na walezi wote kisarawe kuhakikisha wanawapeleka watoto wao wote wa Darasa la awali,msingi na Sekondari wa kidato Cha kwanza leo 08.01.2024.
Akizungumza wakati wa kukagua na kuangalia maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya Katika shule za Sekondari na msingi kwa kata ya kisarawe leo huku akiambatana na mkuu wa idara ya elimu awali na msingi pamoja na kaimu afisa elimu Sekondari amesema
*"Sisi kisarawe tumejipanga kuwapokea wanafunzi wote ambao wanasifa za kuanza shule Mwaka 2024 kwa shule za awali,msingi na Sekondari kisarawe kwa kuwepo na miundombinu ya madarasa,walimu, na vyoo hivyo wanafunzi waje tu alisisitiza*" MHE FATMA NYANGASA
*"MHE DKT SAMIA SULUHU HASSAN amekwisha sema na kuwalipia wanafunzi wote ada za shule hivyo kilichobaki kwa Sasa ni kusoma tu kwa mzazi ni sare na mahitaji mengine hivyo ni kuhimu mzazi ama mlezi kuyasimamia kwa mtoto wake Alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
*"Natoa wito kwa Sasa wiki Hii ya kwanza wanafunzi kuja kwa hiari shuleni ilaa baada ya hapo asiyekuja shuleni na Mwalimu mkuu Hana taarifa tutamfuatilia na kumchukulia hatua maana MHE DKT SAMIA SULUHU HASSAN amekwisha lipia wanafunzi wote shuleni*" alisisitiza MHE FATMA NYANGASA
Nae afisa elimu Sekondari amesema kuwa kwa Sasa Zaidi ya asili 89% ya wanafunzi tayari washawasili shuleni na matarajio ndani ya wiki Hii wanafunzi wote kuwasili shuleni kuendelea na masomo,
*"kwa mujibu wa malengo ya Mwaka 2024 ya kupokea wanafunzi halmashauri ya wilaya kisarawe kwa kata zote 17 shule zetu zote zipo tayari kwa ajili ya masomo na tupo asilimia 89% ya waliokusudiwa kuandikishwa Alifafanua*" MWL MATHIAS HASSANI
Aidha Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya kisarawe MHE FATMA NYANGASA alipata Muda wa kutembelea jengo la utawala la halmashauri ya wilaya kisarawe kwa na kutoa ushauri elekezi ili kumalizika kwa wakati jengo Hilo ili kuanza kutumika kunakotoka na mradi huo kupokea Fedha kutoka Serikali Kuu.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa