KISARAWE YAJIPANGA KUTANGAZA MADINI-COSTA
Na Mwandishi Wetu
KIBAHA
Monesho ya Tatu ya viwanda uwekezaji na biashara mkoa wa pwani yamefunguliwa leo na mkuu wa mkoa wa pwani Mhe Abubakari Kunenge huku wilaya ya kisarawe wakiitumia fursa Hiyo Kuendelea kutangaza kwa wawekezaji wakubwa maeneo ya madini kata ya Kisarawe, Marumbo,Mzenga na Vihingo,
Akizingumza kwa wawekezaji wanaotembelea banda la kisarawe Afisa Biashara ambaye pia Kaimu mkuu wa idara ya Bishara na uwekezaji kisarawe ndugu Joachim Costa alisema kisarawe Ina maeneo mengi ya uwekezaji katika madini ya Kaolin, Yapo mengi na kwa ajili ya Kutengeneza Tiles, Nk na vifaa vya Ujenzi Mbalimbali alisema Costa
"Kwa ujumla kisarawe Imebarikiwa na maneneo ya madini ya Ujenzi mengi mno takriban tarafa zote za kisarawe Zina madini hayo hivyo tupo Hapa kuyatangaza kwa wawekezaji wa Tanzania kupitia maonesho Kama haya Alimalizia Kosta"
"Asilimia kubwa ya madini mkoa we pwani yanapatika kisarawe na pia kwa Wingi na Tena Yale original kabisa na yenye Ubora wa kiwango Cha juu Alimalizia Kosta"
Maonesho haya ya viwanda uwekezaji na biashara Ni ya Siku sita kwa Halmashauri na Wadau Mbalimbali wa viwanda vidogovidogo kuonesha Teknolojia ya viwanda vyao katika usalishaji Mali za viwanda vyao.
Miongoni mwa madini yanayopatikana kwa Wingi kisarawe Ni Kaolin, Limestone, Sandy.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa