Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kisarawe Ndg.Abdallah Dikupatile amewataka maafisa na kamati ya fedha na mipango ya wilaya ya kisarawe kujipanga Zaidi na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani katika vyanzo mbalimbali walivyonavyo sambamba na kubuni mbinu mpya ili kuongeza mapato ya halmashauri.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa vyanzo vya mapato katika kata ya Vihingo kijiji cha kibwemwenda na kata ya Kiluvya kitongoji cha kisopwa ambapo kuna vyanzo vya halmashauri vya mapato vya chimbo la mchanga na kifusi ambavyo huchangia asilimia kubwa ya mapato ya halmashauri.
“Kisarawe kuna vyanzo vingi sana vya mapato ambavyo hutusaidia kuongeza pato la ndani katika ukusanyaji iwapo tutaelekeza nguvu zetu huko na kutupelekea kupata mapato ambayo yatasaidia kuendesha halmashauri yetu pamoja na utatuzi wa usaidizi wa miradi mbalimbali ambayo inaibuliwa katika jamii zetu ambayo tunapaswa kusaidia fedha zinazopatikana katika vyanzo vyetu” Alisema Ndg. Abdallah Dikupatile.
Naye Mtendaji wa kata ya kiluvya Ndg. Mohamed Nundu aliitaka kamati hiyo ya fedha na mipango kisarawe kufuatilia mgogoro uliopo baina ya kisopwa wilaya ya kisarawe na Ubungo wilaya Kinondoni na kuutatua mgogoro uliopo ambao ndani yake kuna chimbo la kifusi ambapo halmashauri ya kinondoni imeweka askari na mashine (POS) ya ukusanyaji mapato katika kizuia cha kisopwa na kupelekea mapato kupotea kwa halmashauri ya kisarawe.
“Waheshimiwa wajumbe wa kamati ya fedha na mipango ,halmashauri ya kinondoni inatuchukulia mapato yetu hapa kisopwa kwa muda mrefu kunakotokana na kuleta wakusanyaji wa mapato na mashine na askari mgambo katika eneo la kisarawe na mipaka ya kisarawe hapa katika chimbo la kifusi cha udongo mloganzila kisopwa ,Hivyo huibia mapato yetu sisi kisarawe”Alisema Ndg.Nundu.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa