KATIKA kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi [CCM ] kwa vitendo halmashauri ya wilaya ya kisarawe kupitia kamati ya fedha imeitaka ofisi ya MHANDISI MKUU WA MAJENGO ya halmashauri ya kisarawe kujenga na kusimamia kwa uweledi miradi yote inayoisimamia kwa kiwango bora na imara cha majengo ya serikali katika sekta ya AFYA na ELIMU Akitoa wito huo kwa niaba ya kamati ya fedha Makamu mwenyekiti wa halmashauri Mhe Amina Ali Lilomo alisema kisarawe kwa mwaka huu wa fedha imekusudia kukamilisha miradi mingi hivyo umakini na ufanisi mkubwa unahitajika ili kuhakikisha majengo na miradi hii inakua na tija na ufanisi kwa jamii ili kuondokana na ukarabati wa mara kwa mara ambao unaweza kuongeza garama za ujenz. jumla ya miradi kumi inakusudiwa kukamilishwa ambayo ipo katika Kata ya Kibuta, Mzenga ,Chole, Maneromango ,Vikumburu ,kisarawe ,Gwata na Msimbu ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani kwa wananchi wa kisarawe pwani
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa