• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Kisarawe District Council
Kisarawe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazigira
      • Afya
    • Vitengo
      • Sheria
      • TEHAMA NA UHUSIANO
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji na Nyuki
    • Programu
      • TASAF
      • UKIMWI
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
      • Vivutio vya Mali kale
      • Vivutio vya Utamaduni
      • Vivutio vya Asili
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Teknolojia
    • Industries
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
      • Huduma za Jamii
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mhe. Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba za Viongozi Mbali mbali

KISARAWE YAPANDA MITI YA KUZALISHA MVUA DAR ES SALAAM

Posted on: April 4th, 2019


 Wilaya ya Kisarawe ni miongoni mwa wilaya 8 za Mkoa wa Pwani na ina ukubwa wa kilomita za mraba 32,407. Wilaya ya Kisarawe imepakana na Manispaa ya Ilala upande wa Mashariki, Kibaha upande wa Magharibi, Wilaya ya Morogoro vijijini kwa upande wa Kusini na Manispaa ya Kinondoni kwa upande wa Kaskazini. Katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira wilaya ya Kisarawe ina misitu yenye usimamizi wa aina tatu ambazo ni Mataji wazi, Hifadhi za vijiji na Hifadhi za serikali kuu.

Aidha pia , Misitu iliyoko katika wilaya ya Kisarawe inasimiwa na mamlaka zifuatazo:-

 HIFADHI ZA SERIKALI KUU

Jedwali namba 1.

Namba
Jina la Msitu
Ukubwa (Hekta)
Mmiliki
1
Hifadhi ya Kazimzumbwi
4,862
Serikali ya Kuu
2
Hifadhi ya Pugu
2,410
Serikali ya Kuu
3
Hifadhi ya Ruvu kusini
35,000
Serikali ya Kuu
4
Hifadhi ya Masanganya
2,899
Serikali ya Kuu

HIFADHI ZA VIJIJI

Jedwali namba 2.

Namba
Jina la msitu
Ukubwa (Hekta)
Mmiliki
1.
Hifadhi ya Nyani
1,006.5
Serikali ya Kijiji
2.
Hifadhi ya Kidugalo
105
Serikali ya Kijiji
3.
Hifadhi ya Msanga sokoni
238.7
Serikali ya Kijiji
4.
Hifadhi ya Kisangire
633.33
Serikali ya Kijiji
5.
Hifadhi ya Mafumbi
1,182.76
Serikali ya Kijiji
6.
Hifadhi ya Sofu
815.75
Serikali ya Kijiji
7.
Hifadhi ya Chakenge
316
Serikali ya Kijiji
8.
Hifadhi ya Kisanga
101
Serikali ya Kijiji
9.
Hifadhi ya Maharage gwata
2670
Serikali ya kijiji

MATAJI WAZI

Hata hivyo, Misitu ya mataji wazi iko kwenye kanda nne ambazo ni:-

Gwata Kidunda hekta 1,911.

Gwata Mzenga hekta 75,200.

Kihare Marui hekta 60,000.

Vikumburu hekta 57,000.

SHUGHULI ZA MAANDALIZI YA VITALU NA UPANDAJI MITI

Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ina vitalu  vitatu,( 3) vya Miche ya miti ambavyo ni: Kisarawe- Bomani,

Mzenga - ofisi ya kata,

Kijiji cha Mtakayo Vitalu hivi  vimezalisha jumla ya miche ya miti 670,000 ya aina mbalimbali miche ya miti  ambayo hutolewa bure kwa wadau wote wanaohitaji kupanda kwenye maeneo yao. Miche inayobakia hupandwa kwenye maeneo ya Taasisi za umma na Misitu ya hifadhi za vijiji, na serikali kuu.

Mkakati wa upandaji miti wa Wilaya ni kupanda miti Milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

Jedwali lifuatalo linaonyesha Mpango wa upandaji miti kwa wadau mbalimbali Jedwali:1  Mkakati wa Upandaji miti 2018/2019

Namba.
Wadau 

Idadi ya miche

1.
Watu binafsi

720,000

2.
Asasi za kidini

200,000,

3.
CBOs

150,000,

4
Wakala wa Misitu Tanzania

100,000.

5.
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe

350,000,

Jumla ya miche ya miti tarajiwa

1,520,000

Halkadhalika, Matarajio yetu ni kwamba miche hiyo ya miti itakayozalishwa itapandwa maeneo mbalimbali kama vile maeneo ya uvunaji wa mazao ya misitu, misitu ya hifadhi, maeneo yaliyo haribiwa na shughuli za kibinadamu kama vile Kilimo na uchomaji mkaa. Miche hiyo itapandwa pia katika Vyanzo vya maji, Hifadhi za misitu za serikali kuu, hifadhi za vijiji, Tasisi za umma, na mashamba ya watu binafsi. Upandaji miti unaofanyika leo ni chachu ya upandaji miti kwenye maeneo mengine ndani ya wilaya yetu.

MAFANIKIO

Mheshimiwa mgeni rasmi, yafuatayo ni baadhi ya mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za upandaji miti wilaya ya Kisarawe.

Uwepo wa vitalu vitatu vya kuzalisha miche ya miti ya aina mbalimbali

Doria za mara kwa mara nje na ndani ya misitu ya Hifadhi.

Uwepo wa wadau wa mazingira mfano WWF

Kuwepo kwa sheria ndogo za uhifadhi na usimamizi wa Misitu.

Uwepo wa kamati za mazingira za vijiji na vitongoji.

Uwepo wa kamati ya Wilaya ya usimamizi wa uvunaji endelevu wa mazao ya misitu. 

CHANGAMOTO. AIDHA pia , zifuatazo ni baadhi ya changamoto tunzokabilianazo kiutendaji.

Uhaba wa vitendea kazi kama gari kwa ajili ya Kusambaza miche ya miti na kufanya ufuatiliaji.

Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya kuendesha Shughuli za utunzaji wa misitu.

 Uchomaji Moto na Holela. Uhaba wa watumishi

Kuongezeka kwa Mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi za Misitu.

Uhaba wa maji ya kumwagilia miche ya miti.

Uelewa  mdogo kwa baadhi ya wananchi kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira MIKAKAT 

AIDHA Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejiwekea mikakati mbalimbali ili kuendeleza juhudi za serikali za kuendeleza na kutunza misitu.

Kuendeleza vitalu vya miche ya miti na kupanda miti kwenye Maeneo yaliyoharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Kuhamasisha wananchi na tasisi binafsi kupanda miti kwenye maeneo yao.

Kufanya doria za mara kwa mara kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kama vile TFS.

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa Mazingira kama vile WWF na TFS

Utoaji wa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Hitimisho

leo hii unapozindua zoezi hili la upandaji miti, usambazaji wa miti unaendelea kwenye maeneo mengine kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yaliyoandaliwa.

 

PANDA MITI IKUTUNZE 

‘’KISARAWE TUNATEKELEZA ILANI YA CCM KWA VITENDO’’

Matangazo

  • Wito Kwenye Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari tarehe 10-11/02/2025 Minaki Sekondari. February 07, 2025
  • Tangazo kwa Umma Kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura February 08, 2025
  • MKITANO WA BARAZA LA MADIWANI April 28, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI NOVEMBA 2021 November 09, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya kabisa

  • NIMEFURAHISHWA NA MMLIVYOJIPANGA KISARAWE CHATANDA NA ZAINABU

    May 08, 2025
  • OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS SERIKALI MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA KISARAWE

    April 30, 2025
  • KISARAWE YAFANYA UTOAJI ELIMU YA DOZI YA NYONGEZA YA CHANJO YA SINDANO YA POLIO(IPV2)

    April 30, 2025
  • KUVUNJWA KWA BARAZA LA MADIWANI KISARAWE UONGOZI WAJIVUNIA KUKAMILISHA MIRADI MBALIMBALI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Kamati ya Fedha kutembelea Ujenzi wa Jengo Jipya la OPD Kisarawe Hospitali
Video

Viungio

  • Utalii wa asili
  • Bima ya Afya (CHF)
  • Historia ya Kisarawe
  • Matukio mbali mbali ya Picha
  • Ukarabati wa Jengo la Upasuaji.
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Kukutana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Maelekezo jinsi ya kutumia Mfumo wa FFARS
  • Orodha ya Madiwani pamoja na Namba za simu

Viungio linganishi

  • OFISI YA RAIS UTUMISHI
  • Baraza la Mitiani ya Taifa
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
  • PPRA
  • Ikulu
  • Ajira
  • Idara kuu ya Takwimu
  • Tovuti ya kupata nakara ya Mshahara
  • Tovuti ya Taifa
  • Bunge
  • Mfumo wa Ununuzi wa Umma NeST
  • Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (ESS)

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Ramani ya Eneo

Kuhusu Sisi

Mawasiliano zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa