Taasisi ya kuhudumia jamii ya Dar es Salaam HOPE 4 YOUNG imetoa misaada lishe mbalimbali kwa jamii ya watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu wilayani kisarawe katika kata ya kisarawe na kazimzumbwi na kituo cha kulelea watoto kilichopo kisarawe.
Akizungumza wakati wa kupokea misaada hiyo Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya kisarawe kwa niaba ya mkurugenzi ndg.Abdalah Masati ameishukuru taasisi hiyo kwa kujitolea kuichagua kisarawe kwa ajili ya kuipa misaada mbalimbali ya ki utu nan a kuweza kunusuru majanga mbalimbali yanayoikumba jamii hiyo katika kupambana na mazingira magumu wanayokumbana nayo.
“Kwa niaba ya wana kisarawe tunasema asante sana kwa msaada huu,Imani yetu msaada huu unaenda kusaidia jamii hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya,na tunaziomba taasisi nyingine ziendelee kusaidia jamii zinazoishi katika mazingira magumu”
Aidha mkurugenzi wa HOPE 4 YOUNG aliushukuru uongozi wa wilaya kwa kukubali kuruhu taasisi kama yake kuja kutoa misaada ya kwa jamii zinazokabiliwa na mazingira magumu
“Ni mara chache sana taasisi kama zetu kuruhusiwa kutoa misaada katika halmashauri kwani kumejengeka taswira ya kuwa taasisi kama zetu huwa zinadharirisha jamii kutokana na misaada tunayotoa,Hivo nashauri taasisi nyingine nazo zije kusaidia jamii maana bado uhitaji unahitajika kisarawe”
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa