KUVUNJWA KWA BARAZA LA MADIWANI KISARAWE UONGOZI WAJIVUNIA KUKAMILISHA MIRADI MBALIMBALI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5
Halmashauri ya Kisarawe imevunja Baraza lake la madiwani lililohudumu kwa muda wa miaka mitano huku ikikamilisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari,msingi na zahanati katika kata 17 ndani ya Kisarawe.
Akizungumza katika kikao cha kuvunjwa kwa baraza la madiwani katika Wilaya hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Mhe, Zuberi Juma Kizwezwe amesema uongozi wa Halmashauri hiyo Mwaka 2020-2025 umeweka historia katika nchi hii kwa kutekeleza miradi mingi mbalimbali katika kipindi hicho cha miaka mitano.
“Waheshimiwa mtembee kifua mbele mjue mmeweka historia na rekodi ziko wazi ni halmashauri ya Bora kuwa na uzimamizi mzuri wa Kusimamia fedha za Serikali na kuwa na baraza tulivu katika nyaja mbalimbali Halmashauri imeweka historia”. Amesema Mhe.Kizwezwe
Akizungumza katika baraza hilo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Bw Nyahori Mahumbwe amewataka madiwani kuendeleza upambanaji waliouonesha kwa kipindi chote walichofanya kazi ndani ya halmashauri hiyo.
“Hakika uongozi uliopo chini ya Mheshimiwa Zuberi Juma Kizwezwe umeiongoza na kulisimamia vizuri baraza la madiwani na kuleta ufanisi mkubwa”. Amesema Bw Nyahori Mahumbwe,
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe DC.Petro Magoti amesema kuwa mpaka sasa miradi ya mingi imeweza kutekelezwa katika Wilaya hiyo hasa kwenye miundombinu ya barabara ambapo maeneo mengi yalikuwa ni rahisi kuathiriwa na mvua pindi zinaponyesha.
“Nimefanya kazi na menejimenti ya Mkurugenzi, mnaondoka mkiwa mmeacha safu nzuri sana ya Halmashauri na yatatekelezwa yale ambayo sisi sasa tunaamini hata yale ambayo mnayaacha hayajakamilika yatakamilika yakiwa salama na ubora unaotakiwa”. Amesema DC.Magoti
Amewapongeza Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe Zuberi Juma Kizwezwe kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye maneneo Yetu.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa