LUCKY CEMENT WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI KISARAWE.
Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Lucky Cement kilichopo kata ya Kazimzumbwi Wilayani Kisarawe kimetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo Wilayani Kisarawe.
Katika tukio la makabidhiano ya vifaa hivyo kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Afisa uhusiano wa kiwanda cha Lucky cement ndugu Ally Mohamed amesema wamekuja kutoa vifaa hivi kwa ajili ya kuitikia wito uliotolewa awali wa kuchangia kuboresha elimu kwa wanafunzi uliotolewa na viongozi wa Wilaya na Halmashauri .
‘’tumeitikia wito wa kuchangia vifaa hivi ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na uongozi katika kuboresha elimu kwa wanafunzi wetu kwani hawa wanafunzi watakaophitimu baadae wanaenda kuhudumia wananchi nchi nzima hivyo naomba na makampuni mengine yaje kuunga mkono juhudi za mheshimiwa mkuu wa Wilaya katika kuchangia na kuboresha elimu’’ Amesema ndugu Ally Mohamed
Wakati anapokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Happiness William Seneda ameshukuru na kusema kuwa mara nyingi kiwanda cha saruji wamekuwa na muitikio mkubwa kwenye kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanyika hapa wilayani na wakati wote wamejitokeza kuchangia kuanzia ngazi zote za vitongoji,kata na wilayani hivyo amewashukuru sana .
Katika makabidhiano hayo kiwanda cha Saruji cha Lucky Cement wametoa msaada wa kilogramu mia mbili(200) za unga wa sembe , kilogramu mia mbili(200) za mchele,kilogaramu mia moja (100)za unga wa ngano,kilogamu mia moja(100) za sukari,mafuta ya kula lita sitini (60) na katoni za maji hamsini (50)
Mnamo tarehe 7/10/2017 wilaya ya kisarawe ilifanya Harambee ya kuchangisha fedha na vifaa kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuwaweka kambi wanafunzi wa kidato cha nne wanaofanya mitihani ya kumaliza elimu ya sekondari kwa mwaka huu.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa