Kesho siku ya Jumanne tarehe 19.06.2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe itaadhimisha kilele cha siku ya mtoto Afrika.
Maadhimisho hayo kiwilaya yatafanyika katika Kijiji cha Sungwi Kata ya Masaki kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Sungwi na yanatarajiwa kuanza saa mbili asubuhi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Mkuu wa Wilaya ya KIsarawe Mheshimiwa Happiness Seneda.Kauli mbiu ya mwaka 2018 kuhusu maadhimisho haya ni ‘’KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA ,TUSIMWACHE MTOTO NYUMA’’
WOTE MNAKARIBISHWA
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa