MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA KISARAWE WAPITISHA BAJETI YA TSH 41,028,607,050,48 KWA MWAKA WA FEDHA 2024-2025.
KISARAWE PWANI
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe leo 15 Februari, 2024 limeridhia na kumepitisha Mpango na Bajeti ya Tsh. Billion 41.028,607,050.48kwa mwaka 2024/2025. Maamuzi hayo yamefanyika wakati wa mkutano maalumu wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Fedha hizo zitatumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali za utoaji huduma, utawala na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri , Afisa Mipango, Bw. Deogratius Lukomanya ameeleza kuwa bajeti hiyo imezingatia miongozo ya kitaifa na halmashauri. Miongozo hiyo ni pamoja na kupokea mapendekezo kutoka kwa wajumbe mbali mbali katika ngazi ya Wilaya, Kata, Vijiji, Vitengo na Divisheni za Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
Aidha, Bw. Lukomanya amefafanua kwamba katika rasimu hiyo ya Bajeti , kiasi cha Bilioni 4,810,513,000.00ni fedha zitatokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri, kiasi cha shilingi Bilioni 22,927,604,104.00 ni ruzuku ya mishahara ya Watumishi, kiasi cha shilingi milioni 1,498,806,000.00 ni ruzuku ya uendeshaji wa ofisi ( OC) na kiasi cha Bilioni 12,273,452,500,00 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali kuu,
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri MHE ZUBERI KIZWEZWE katika hotuba yake amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmasahuri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg BEATRICE DOMINIC kuendeleza jitihada alizozianzisha katika kutekeleza majukumu ya halmashauri na kumtaka kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati ili wananchi wafurahie matunda ya nchi yao Tanzania “nina imani kubwa na wewe na sina mashaka na utendaji kazi wako” amesema MHE KIZWEZWE,
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Ndg BEATRICE DOMINIC amefafanua kuwa amebaini kuwa vyanzo vingi vya mapato haviwekwi kwa uhalisia na hata vinavyowekwa havifikii malengo. Hivyo, amewaomba Waheshimiwa Madiwani na kuwataka watendaji wa halmashauri kuwa kitu kimoja na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Pale ambapo hatufanyi vizuri tuambiwe pasipo kuoneana haya na tunapokosea tukosolewe kwa kuwa wote tunaijenga halmashauri moja" alisisitiza Ndg BEATRICE DOMINIC
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kisarawe Komred Khalfani Sika alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia vyema ilani ya CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KWA vitendo Kisarawe Katika Miradi.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa