MADIWANI WAWATAKA WATUMISHI KISARAWE KUWA WAADILIFU KATIKA KUKUSANYA MAPATO
Na
Mwandishi Wetu.
Babaraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Kisarawe 29.08.2023 Kwa kauli moja wamewataka watumishi kukusanya mapato huku wakitanguliza Uadilifu na umakini Bila kumuonea mtu wakati wa Zoezi hilo,
Akizungumza wakati wa Kufunga kikao maalum cha kamati ya fedha Utawala na Mipango Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe Mhe Mohamed Lubondo alisema kuwa ni Vyema watumishi wa Kisarawe wakatanguliza umakini na Utu wakati wa Zoezi la Kukusanya mapato ya Halmashauri bila Kutumia nguvu na vitisho Kwa Raia,
"imefikia hatua wananchi wakiwaona wakusanya mapato huko vijijini wanawaogopa Sasa hili naomba Kwa nyie lisiwepo najua halipo ila lisiwepo maana halileti ubinadamu na urafiki uliopo baina ya raia na watumishi alifafanua Mhe Lubondo"
"Tunawaagiza mwaka huu wa fedha kuongeza kasi ya kukusanya mapato lakini tunataka mapato ya Haki na yenye amani na upendo sio Kwa fujo na Ugomvi sisi Kisarawe tuna vyanzo vingi na Bora ambavyo vitazalisha na kuongeza mfuko wetu hapa Halmashauri Alisisitiza Mhe Lubondo"
Katika Baraza miongoni mwa agenda zilizojadiliwa ni pamoja na Taarifa ya mizania ya Hesabu,Taarifa ya Matumizi,Taarifa ya Mtaji,Taarifa ya Bajeti,Taarifa ya Fedha.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa