Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya kisarawe ambaye pia ni diwani wa kata ya maneromango Mhe Abdallah Dikupatile awataka na kuwaomba mafundi wavijiji ambao wanatumika katika ujenzi wa miradi ya serikali na mashirika ya umma kujenga miundo mbinu katika vijiji vya kisarawe kuwa na uzalendo wa hali juu ili kulinda na kuokoa fedha za miradi ya serikali na kuweza kutumika sehemu nyengine fedha zinazookolewa kulingana mradi wa kwanza
Akitoa wito huo wakati wa kuhamasisha jamii kushiriki kwa vitendo katika hamasa ya ujenzi wa miundo mbinu ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu ya choo katika shule ya msingi Madugike maneromango kisarawe
‘’Mafundi wa vijijini mna nafasi kubwa ya kuokoa fedha za miradi ya serikali na kupelekea kupatikana kwa mradi mbadala iwapo tu mtakua wazalendo maana nyie huwa mnajua vyema kuwa ni sehemu ya kupunguza gharama ya kumlipa fundi kutoka mbali hivyo naomba mtusaidie kuokoa katika miradi hii ya serikali’’ alisema Dikupatile
Jumla ya shilingi milioni Arobaini na Sita na laki Sita zimetolewa na serikali kupitia mradi wa (Pay for Result P4R) kwa shule hiyo ya madugike ili kuboresha miundo mbinu yake hapo maneromango.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa