Tarehe 06/07/2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu. Beatrice R. Dominic amefungua Mafunzo ya Mfumo wa Anuani za makazi kwa watendaji wa Vijiji na Kata ambapo washiriki wa mafunzo wamefundishwa moduli mbalimbali za mfumo huo pamoja na namna ya Utoaji wa Barua za Utambulisho kidijitali.
Akizungumza na washiriki hao Ndugu. Beatrice R. Dominic amewahimiza Watendaji kuwahudumia wananchi kikamilifu kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amewaelekeza watendaji hao kukusanya mapato ya Halmashauri,Kuzuia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kusimamamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Mkuu wa Idara ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi. Sabra Mwankenja amewahimiza watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utoaji wa huduma. Pamoja na kuwahimiza kuzingatia yote waliyofundishwa katika Mfumo huo wa Anuani za Makazi.
Naye Mratibu wa Anuani za Makazi Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bw. Nsanganiye J. Bilinzozi amewasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatekeleza zoezi hili muhimu la utoaji huduma kidigitali.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa