Mkuu wa wilaya ya kisarawe ameipongeza Ofisi ya kata ya Maneromango kwa kujali na kufuatilia kwa vitendo katika kuwatatulia matatizo na chanagamoto za wafanya biashara wadogo wadogo hasa kwa serikali ya kata na kijiji kuwafuatilia katika kuwapatia vitambulisho vya wafanya biashara vinavyotewa na ofisi ya mkurugenzi wilaya kwa kuratibiwa na idara ya biashara kisarawe,
Akitoa pongezi hizo maneromango wakati alipokua katika ziara ya kuzungumza na wananchi katika uhamasishaji wa Ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo yanayojengwa na mradi wa lipa kulingana na matokeo (Pay for Result P4R) ambao unahitaji kwa nguvu kubwa uwepo wa wanachi kuelewa na kufuatilia kwa vitendo miradi iliyopo katika vijiji vyao,
‘’Ndugu zangu wa kisarawe nimefurahishwa sana na mwamko wa wafanya biashara wa hapa maneromango pamoja na ofisi ya kata kwa ujumla katika kusimamia na kuhakikisha kua kila mfanya biashara wa hapa anapata kitambulisho ili aweze kufanya biashara na kuzalisha kwa kujenga taifa lenye wafanya biashara ambao wanalipa kodi kwa hiari na upendo bila kushurutishwa,‘’
DC Mwegelo ametoa wito kwa mafisa wa serikali wa vijiji na kata nyengine za kisarawe kuhakikisha kuwa wanawafuatilia na kuwafuata wafanya biashara huko waliko ili wawapatie vitambulisho hivyo na serikali kupata kodi stahiki kwa wakati maana jamii kubwa ya wafanya biashara hawapendi kulipa kodi ,
’’Nawagiza watendaji na mafisa wote wa serikali wa ngazi ya tarafa, kata na kijiji kuhakikisha kuwa wafanya biashara wote waliopo kwenu wanafikiwa na kupatiwa vitambulisho kabla ya kuja kwa awamu ya pili ya kutolewa vitabulssho,’ alisisitiza Dc Mwegelo
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa