MAONYESHO ya wiki ya Viwanda Mkoa wa Pwani yamefanyika Kibaha kwa kushirikisha Wilaya zote Saba za Mkoa wa Pwani kwenda kuonyesha na kutangaza Bidhaa za Viwandani walizonazo na kutangaza fursa za maeneo tengefu ya uwekezaji ya viwanda kilimo na makazi kwa lengo la kuwarahisishia na kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza katika Wilaya zao bila usumbufu wa aina yoyote ile kulingana na aina ya uwekezaji na uanzishaji wa kiwanda katika maeneo tengefu yanayohitajika hayo yote yakiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha MAPINDUZI CCM Chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa sera ya HAPA KAZI TU
KISARAWE ni miongoni mwa Wilaya zilizopata fursa ya kushiriki katika maonyesho hayo ya wiki ya Viwanda mkoa wa Pwani kwa kuonyesha na kutangaza fursa zilizopo kwa wawekezaji na wajasiriliamali waliopo na wanaotaka kuwekeza kuja kuwekeza kisarawe kutokana na kuwapo kwa dawati la uwezeshaji na uwekezaji kisarawe lenye lengo la kukuza na kutangaza fursa za uwekezaji katika maeneo ya kilimo na mifugo,utali,makazi na viwanda
UWEKEZAJ SEKTA YA KILIMO jumla ya eneo linalofaa kwa kilimo ni ekari 353,500 hekta zinazotumika kwa kilimo ni 30,000 sawa na asilimia 8.5 Banda la Kisarawe liliiitangaza sekta hii kwa kusema uwepo wa Ardhi yenye rutuba na udongo wenye kukubali kwa kilimo cha mazao ya Biashara na Chakula Kisarawe ni vyema kila Mjasiriamali na mwekezaji afikirie kuja kuwekeza katika sekta hiyo kwa ufanisii maana hatapata hasara miongoni mwa mazao yanayokubali kwa uzuri na kutokuadhiriwa na magonjwa ni Mihogo ,Ndizi Mtama,Nazi,Korosho na Viazi Mviringo hasa Kata ya Mafizi,Marumbo,Marui Gwata, Bwama nk
UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO
kutokana na kukua kwa mji na maeneo ya Kisarawe imetenga eneo maaalum la kufugia wanyama na kama Ngombe,Mbuzi na Kondoo sambamba na kutenga eneo la machinjio ya kisasa ya wanyama lililopo katika Kata ya Kazimzubwi Kitongoji cha Vigama ambalo ni kilomita 10 tu kutoka Pugu mnadani ambapo sasa ndio ulipo mnada wa Dar es salaam mifugo ambayo itapelekea kupatikana kwa kiwanda cha Ngozi na madawa kunakotokana na uwepo wa mifugo ya kutosha Kisarawe.
UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA VIWANDA NA MAKAZI, Katika kukabiliana na ongezeko la watu na makazi na ujenzi holela wa miji isiyopangwa duniani Wilaya imetenga eneo makhusi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na makazi katika kata ya Kazimzubwi kwa ajili ya Viwanda na kata ya Kiluvya kwa ajili ya makazi kitongoji cha kilunya madukani, viwanja hivyo vipo vya aina tatu kulingana na matumizi na mahitaji ya mteja .
UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UTALII Hii ni fursa ambayoo ni adhimu na yenye kutoa na kuchangia fedha za kigeni kwa wingi na kutoa ajira kwa wadau wenye kujihusisha na utalii kisarawe ina msitu mkubwa wa asili Kama kazimzumbwi ,kola,na hifadhi ya ruvu na taifa ya Sadani ambayo kwa asislimia kubwa ina wanyama wenye kuonekana na wasiokua na madhara sana kwa binadamu ambao ni kivutio cha utalii mfano wa wanyama hao ni Simba,tembo,swala,punda milia ,na wengine wengi ambao wanapatikana katika misitu hiyoo sambamba na uwepo wa mapango ya popo, ndege,kambi ya kinyanyiko ya utalii, na miti asili ya aina mbalimbali kama Mkongo,Mninga Mtondo. Hata hivyoo uwepo wa fursa ya uanzishwaji wa maduka ya vifaa vya utamaduni na pia utalii wa ndani na vituo vya utalii.
MAONYESHO HAYA yalipata fursa ya kutembelewa na wageni waalikwa kwa lengo la kuhamasisha ujenzi na uimarishaji wa viwanda vya mkoa wa pwani kama vile Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Mungano wa Tanzania Mhe DR TULIA , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe Selemani Jaffo, Waziri wa Nishati na Madini Dr Kalimani, Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Mhe MWIJAGE,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu, WOTE KWA PAMOJA walisifu mbinu iliyootumika na viongozi wa mkoa wa pwani na wilaya zake kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM kwa kuanzisha maonyesho haya na kutoa wito kuendelea kila baada ya miezi mitatu badala ya kua kila mwaka mmoja ili kuvipa fursa viwanda na vyetu na wajasiria mali wetu kuonyesha bidhaa zao kwa wadau na watanzinia kwa ujumla na jumla 245 walitembelea banda la halmashauri ya kisarawe na 33 walionyesha nia ya kuwekeza kisarawe katika sekta ya kilimo,mifugo ,ufugaji nyuki,elimu,maziwa,viwanda na utalii.
KAULI MBIU ya wiki ya viwanda ni ‘’VIWANDA VYETU UCHUMI WETU’’
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa