Kisarawe ,Pwani
28/12/2020
Leo tarehe 28/12/2020 Mara baada ya Mapumziko ya sikukuu ya Krismass Mhe Jafo afanya ziara ya kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari Kisarawe ambayo inajengwa kwenye kata ya Kazimzumbwi.Mara baaada ya kuwasili Mhe waziri alipokea taarifa fupi toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ndugu Musa Gama kuhusu hatua za ujenzi zilipofikia na taarifa ya upokeaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza.Ndugu Gama alisema mpaka sasa hakuna mwanafunzi aliyefaulu atakayekosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza.Katibu Tawala ndugu Mwanana alimkaribisha Mhe. Jafo ili kuongea machache kisha kuelekea eneo la Shule inapojengwa. Katika ukaguzi huo Mhe. Waziri Jafo aliwapongeza wanaosimamia ujenzi kwa kufikia hatua nzuri. Hata hivyo Mhe. Jafo aliwasisitiza waongeze kasi ya ujenzi ili ifikapo tarhe 11/01/2021 ujenzi uwe umekamilika na wanafunzi waanze kutumia majengo hayo. Mpaka sasa ujenzi unaendelea kwa kujenga Madarasa,maabara,ofisi za walimu ,Bwalo la chakula,Chumba cha TEHAMA na Jengo la Utawala.
Mhe Jafo ameridhishwa sana na hatua hiyo na kuwaagiza watendaji na Wanakijiji kutoa ushirikiano na kulinda mali zote zinazotumika katika ujenzi wa shule hiyo.
Aidha wakati Mhe. Jafo akiongea na wananchi aliwatoa hofu kwa kuwaambia kuwa shule hiyo ni maalumu kwa watoto wa kisarawe na sio watoto kutoka Mikoa mingine.
Pamoja na ziara ya kukagua ujenzi wa shule ya sekondari kisarawe Mhe Jafo ambaye pia ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi Kupitia chama cha Mapinduzi alipata nafasi ya kuongea na watumishi wa Taasisi za Umma mbalimbali pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe.
Kwanza aliwashukuru watumishi kwa kumchagua kuwa Mbunge wao pia kumshukuru Mhe.Rais John Magufuli kwa kumchagua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Baada ya shukrani hizo Mhe Jafo alitoa maelekezo yafuatayo:
Mwisho Mhe Waziri Jafo alitoa pole kwa msiba wa baba yake Mzazi Mhe. Mkuu wa Wilaya Jokate na kuwashukuru kwa kushiriki hatua zote hadi kumpumzisha Marehemu huko Mbinga.Waziri aliwataka watumishi wanapoanza mwaka 2021 wakaanze na nguvu mpya wakisahau changamoto zote za mwaka 2020.
Sambamba na hilo Mwenyeki wa chama cha Mapinduzi Ndugu Sika aliwashukuru watumishi kwa kufanya vizuri kwenye kazi zao na kuwataka waendelee na kuongeza bidii huku wakipunguza maneno yasiyoleta maendelee kwa wilaya yetu.
Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ndugu Zuberi Kizwezwe alimshukuru Mhe.Jafo kwa kuja kuongea na watumishi na kuahidi kuwa yote aliyoyaelekeza atakwenda kuyasimamia na kuhakikisha yanatekelezeka.Pia alisema atatoa ushirikiano wa kutosha kwa watumishi ili kufikia malengo chanya ya Halmashauri.
Picha zaidi bofya hapa
Imetolewa na Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO(W)
Kisarawe.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa