Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilaya ya Kisarawe kwa kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo na kupokea taarifa za miradi inayotekelezwa kwa mujibu ya ilani ya chama cha mapinduzi(CCM). Akiwa kisarawe Mheshimiwa Makamu wa Raisi alikagua na kupokea tarifa ya mradi mkubwa wa maji ya kutoka bomba kuu la maji kutoka Kibamba kuelekea Kisarawe na kukagua ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji kiasi cha lita milioni sita unaoendelea eneo la Mnarani Kata ya Kisarawe. Aidha Mheshimiwa Samia alipata muda wa kukagua ujenzi wa barabar za lami na kusalimiana na wananchi wa kisarawe ambao walifika kumlaki na kupokea salamu zao pamoja na kuwafikishia salamu za Rais kwa wakazi wa kisarawe katika kusimamia ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuwaondolea kero zinazowakabili wananchi. Baadae Mheshimiwa makamu wa Rais alitembelea kiwanda cha kuzalisha kilichopo kata ya Kazimzumbwi na kukagua uzalishaji pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili ambapo uongozi wa Kiwanda walimweleza changamoto ya barabara inayoziunganisha Wilaya ya Kisarwawe na Mako Makuu ya mkoa ambayo waliomba iboreshwe ili iweze kutumika katika kusafirisha bidhaa zao.
Aidha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani ameutaka uongozi wa kiwanda cha Saruji kuongeza uzalishaji ,kuongeza ubora na kupunguza bei hiyo sokoni ili kuwezesha wananchi kumudu gharama za ujenzi zinazotumia saruji.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alielekea Tarafa ya Maneromango ambapo alitmbelea Kituo sha afya cha Maneromango ambapo ujenzi wake uligharimu kiasi cha shilingi milioni mia tano na kupokea Msaada wa vifaa tiba kutoka Benki ya NMB.
Pia Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania alitembelea shule ya Sekondari ya Maneromango ambayo nia ya kidato cha tano na sita na kukagua bweni la Wasichana,kusikiliza taarifa za Maendeleo ya shule,kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndugu Mussa Gama kuhusu operesheni maalum ya kuborehs kiwango cha ufaulu kwa jina maarufu la OPERESHENI ONDOA ZERO.
Makamu wa rais aliambatana na mawaziri wa Maji mheshimiwa Profesa Makame Mbalawa,Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe,Naibu wa ziri wa Nishati Mhe.SubIra Mgallu,Naibu Waziri wa Kilimo mhe, Omar Mgumba ,Naibu Waziri wa ujenzi Mhe.Nditiye ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo,Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Ndugu Mussa Gama.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa