"MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO OR-TAMISEMI AKAGUA MIRADI YA ELIMU SEKONDARI KIMANI NA JENGO LA UTAWALA ATOA PONGEZI KWA MKURUGENZI MTENDAJI KISARAWE KWA KUSIMAMIA MIRADI KWA UFANISI NA UBORA
KISARAWE PWANI
Mkurugenzi wa Sera na Mipango OR-TAMISEMI Ndg JOHN MIHAYO CHEYO amefanya ziara maalumu ya ukaguzi wa Miradi ya Elimu Sekondari na Jengo la utawala la Wilayani Kisarawe 22.12.2023.
Akitembelea miradi mbalimbali Hiyo Ndg JOHN MIHAYO CHEYO amesema kuwa Lengo la ziara hii ni kuhakikisha kuwa Wana-kisarawe wanapata huduma ya Elimu bora, Sambamba na kuonesha kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Elimu na Utawala Kisarawe kupitia Fedha mbalimbali zinazoletwa na Kusimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji Kisarawe.
Aidha katika ukaguzi Huo wa miradi ya kimani na Jengo la utawala la Kisarawe pia alikagua hali ya ujenzi wa Miundombinu ya Bweni,Bwalo na Vyoo vya shule ya kimani Sekondari na kupongeza kwa jitihada walizotumia za kusimamia vyema ujenzi wa jengo la utawala na ujenzi wa Madarasa,Vyoo,Bweni,na Bwalo katika shule ya kimani
Sambamba na hapo alisisitiza mambo Muhimu ya kuzingatia ili Miradi iishe kwa Wakati ikiwamo kuendelea zaidi kutoa ushirikiano na usimamizi wa Mzuri Kama wa Awali,
Hi Miradi Kwa Sasa ipo hatua za mwisho Kumaliza ila nimevutiwa Sana na usimamizi Mzuri wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kisarawe katika Miradi hii hivyo nashauri kuendelea na utekelezaji wa Miradi hii kufika asilia Mia Moja asisitiza Ndg JOHN MIHAYO CHEYO,
Katika hatua nyingine, Ndg JOHN MIHAYO CHEYO amesitiza juu ya adhma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya kila mwanafunzi anapata Fursa ya kusoma sambamba na kutunza miundombinu yote ya Elimu pamoja na Watumishi kufanya Kazi katika Mazingira mazuri ya majengo na Kuboresha utoaji huduma kwa kuwahudumia wananchi katika Mazingira Bora kwa Kuboresha majengo ya utawala Nchini,
Aida kwa hatua nyengine alimpongeza mkurugenzi mtendaji kwa kupanga bajeti ya mapato ya ndani kumalizia miradi mbalimbali ya halmashauri ikiwemo mradi wa bwalo katika shule ya sekondari ya kimani alipongeza mkueugezi wa sera na mipango Ndg JOHN MIHAYO CHEYO
Mwisho,Ndg JOHN MIHAYO CHEYO amesisitiza waliopewa dhamana za kutekeleza miradi ya Elimu Wilaya ya Kisarawe kufanya kazi kwa ufanisi, ubora na kwenda na wakati ili kukamilisha miradi husika.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango OR-TAMISEMI ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Ndg. BEATRICE DOMINIC Kaimu wa idara ya ujenzi na Miundombinu Wilaya Kisarawe Eng Leonard Mashaka,Mkuu wa idara ya Mipango Ndg Deogratius Lukomanya,Mkuu wa idara ya Elimu Sekondari Mwl Edith Fue, Afisa Vifaa Sekondari Slo Hassan Mathius.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa