Mkuu wa Wilaya Kisarawe Mhe,Happiness Seneda Wiliam azindua zoezi la la upigaji chapa wa mifugo siku ya tarehe 25/10/2017 Kijiji cha Mafizi Kata ya Mafizi.Awali zoezi hili kwa awmu ya kwanza lilianza tarehe 18/09/2017 hadi tarehe 04/10/2017 ambapo Ng’ombe 11,939 walipigwa chapa na kusajiliwa katika daftari la mifugo la kila Kijiji kwa namba yake,Vijiji ambavyo vilifikiwa katika awamu ya kwanza ni Gwata,Mihugwe,Nyani na Ving’andi.
Awamu ya Pili ya zoezi hili itahusisha Vijiji 19vilivyopimwa na kutenga maeneo ya malisho ya mifugo katika Kata za Chole,Kurui,Marui,Mzenga na Vikumburu.
Aidha siku ya zoezi hili Mkuu wa Wilaya alizindua jengo la ofisi ya Lushu Ranch CO.LTD lililopo Kijiji cha Mafizi katika eneo la mfugaji Ndg Charles Mabula ambaye ni mfugaji wa mfano katika Wilaya ya Kisarawe na amekuwa akishiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya mifugo Kikanda na Kitaifa na kujipatia Tuzo ya mshindi wa kwanza kwa miaka mitatu mfurulizo 2015,2016 na 2017 huko Nzuguni Dodoma.
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa