Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo Amefanya ziara katika kiwanda cha Saruji cha Lucky Cement kilichopo kata ya Kazimzumbwi Wilaya ya Kisarawe.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Jokate ambaye aliongozana na kamati ya Ulinzi ya Wilaya na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Ndugu Hafidh Mohamed ameweza kupata maelezo namna ya uendeshaji na uzalishaji unavyoendelea kiwandani hapo.
Akitoa maelezo juu ya uendeshaji na uzalishaji wa kiwanda hiko Meneja wa kiwanda hicho amesema uzalishaji unaendelea na changamoto zilizopo ni kukatika katika kwa umeme na wameomba malighafi zinazotumika kwenye uzalishaji wa saruji ziwe zinapatikana Kisarawe.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao na changamoto zinazowakabili zitashughulikiwa ikiwamo ya umeme na kusisitiza kuendelea na uzalishaji kwa kiwango kikubwa ili hatimaye serikali ipate kodi kwa ajili ya kuendeshea shughuli mbalimbali za kijamii
kwa habari picha bonyeza hapa
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa