MSIWAFANYIE UPANDIKIZAJI WAWEKEZAJI NA WADAU KATIKA ARDHI-JK KIKWETE
Na
Mwandishi Wetu
Rais Mstaaafu wa Tanzania awamu ya Nne Mhe Dr Jakaya Kitwete leo 06.10.2022 ametembelea mabanda Mbali Mbali katika Maonesho ya Viwanda, Biashara na uwekezaji mkoa wa Pwani Wilaya kibaha huku akitoa wito kwa Wizara na Taasisi za serikali kuacha tabia ya kuwasumbua Wawekezaji pindi wanatotaka kuwekeza katika Uchumi na Ardhi kuendana na kauli ya Zilongwa zitendwa kwa kutokuwafanyia tabia ya Upandikizaji yaani umiliki Zaidi ya mmoja eneo la Ardhi,
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Maanda ya Maonesho ya bidhaa katika Banda la Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi alikemea tabia ya baadhi ya Mafisa wasio waminifu kwa serikali kwa tabia ya kuuza maeneo ya uwekezaji na makazi Mara mbilimbili na kuleta kero kwa Mwekezaji na Raia,
"Hivi nyie Hampimii na kuuza viwanja na maeneo ya uwekezaji hamuuzi kwa kubandia bandi viwanja kwa Mwekezaji Zaidi ya mmoja huku akionyesha ishara ya mayele aliuliza Dr Kikwete*"
" Tabia hii ya kuuwauzia Watu viwanja mtu ama Tasisi zaidi ya mmoja huleta Taharuki sio nzuri na kurudisha Nyuma maendeleo Baada ya mtu kutaka kuwekeza ama Kujenga Sasa anakua Muda wote anatafuta suluhishi la Ardhi hii Hapana alimalizia Dr Kikwete"
"Pwani tuna Ardhi nzuri na salama Naomba tutumie fursa hiyo kwa maendeleo na sio vinginevyo na pia tutumie fursa ya Usalama na ulinzi wa maeneo yetu kwa raia na wawekezaji wetu Pwani"
Aidha pia alizitaka Tasisi nyengine za serikali zinazohusika na Masuala ya maendeleo na uwekezaji Kama na Kutoa ruhusa za maeneo Kama Osha,Zimamoto, T.R.A Ruwasa, T.I.C Tanesco Nk kutekeleza majukumu Yao kwa mujibu wa sheria ili kuvutia wawekezaji kwa Ufanisi wa Maombi pindi wanapowasilisha kwao kwa Muda mchache Kama mnavyowambia Kuwa waje kuwekeza Basi iwe Hivyo na sio vinginevyo,
"Nimefika pale BRELA nimeuliza kusajili kampuni Ni Muda gani nachukua kukamilika nikajibiwa Kuwa Ni Siku Nne Kama kweli hiii ipo vizuri ninawapongeza na inachochea maendeleo Hivyo badilikeni nataka iwe Kama wazaramo wanavyosema Zilongwa zitendwa kwa Pwani alimalizia Dr Kikwete"
Nae kamishna wa Ardhi msaidizi mkoa wa pwani ndugu Hussein Sadiki alisema Kwamba,
"Tunawatoa hofu watanzania wote kwa ujumla kwa Sasa Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Mkuranga kibaha na kibaha mji na chalinze tumeanza kuboresha umiliki wa Tarifa za umiliki kisasa Hivyo hakitakua na upandikizaji wa Umiliki na Mwaka wa Fedha wa mwakani tunatgemea kuendelea kwa Wilaya nyengine yote hii Ni kuboresha na kuondosha Matatizo mbalimbali ya Umiliki Ardhi alimalizia Sadiki"
Hakimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Haki zote zimehifadhiwa